JW LUGHA
Mambo Mbalimbali Kuhusu JW Lugha
Lugha Zinazopatikana
Kiarabu, Kiindonesia, Kirusi, Kibengali, Kiitaliano, Kihispania, Kichina cha Kikantoni (cha Kitamaduni), Kijapani, Kiswahili, Kichina cha Kimandarin (Sahili), Kikorea, Kitagalog, Kiingereza, Kijerumani cha Low, Kithai, Kifaransa, Kimalay, Kituruki, Kijerumani, Kimyanmar, Kivietnam, Kihindi, Kireno.
Ina Habari Kuhusu Huduma
Maneno yaliyo katika programu ya JW Lugha yanahusu kuhubiri, kufundisha, na msamiati wa Biblia. Trakti kadhaa zilizopangwa zinapatikana ili uweze kulinganisha lugha yako na lugha unayojifunza.
Njia Mbalimbali za Kujifunza
Soma maneno na maelezo katika lugha yako, kisha ulinganishe na lugha unayojifunza
Msikilize mwenyeji akitamka neno mojamoja, fungu la maneno, au chapisho
Tazama video kuhusu huduma katika lugha unayojifunza
Jifunze ukitumia picha
Tambua jinsi maneno mbalimbali yanavyoathiri muundo wa sentensi katika kuonyesha Sarufi
Fanya mazoezi ukitumia mbinu mbalimbali za kujifunza
Tazama: Chagua tafsiri ya neno unaloona
Linganisha: Chagua maneno yanayofanana
Sikiliza: Chagua tafsiri ya neno unalosikia
Kadi za Kumbukumbu: Fikiria tafsiri ya neno unaloona
Somo la Kusikiliza: Sikiliza maneno yakisomwa kwa sauti katika rekodi ya kusikiliza yenye sehemu zinazosimama kwa muda ili ufanye mazoezi
Panga Habari Kulingana na Mapendezi Yako
Hifadhi picha na maneno unayopenda ili uyapate haraka
Ongeza au upunguze mwendo wa sehemu ya kusikiliza maneno
Kwa lugha ambazo hazitumii herufi za Kiroma, unaweza kuchagua kuona maneno yaliyotoholewa katika herufi za Kiroma
Pakua habari ili uzitumie bila Intaneti
Tumia nafasi kidogo kwenye kifaa chako kwa kupakua video zenye ubora mdogo
Kubadili Maandishi Yawe Katika Kiroma
Kwa lugha ambazo hazitumii mfumo wa maandishi ya Kiroma, maneno yanaonyeshwa katika Kiroma pia.
Utegemezo
Ukipata matatizo unapotumia JW Lugha, tafadhali jaza na utume fomu ya kutoa msaada inayopatikana katika Tovuti yetu.