Awamu ya 7 ya Picha za Uingereza (Septemba 2018 Hadi Februari 2019)
Katika awamu hii ya picha, utaona jinsi ujenzi ulivyoendelea katika ofisi mpya ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Uingereza kati ya Septemba 2018 na Februari 2019.
Septemba 25, 2018—Makazi A
Kikosi cha mafundi wakichimba kwa kutumia mashine mbili ili waingize sehemu kubwa ya bomba kuu. Jengo la Ofisi linaonekana kule nyuma.
Septemba 26, 2018—Jengo la Kusini la Uzalishaji
Wajenzi wakitengeneza upande wa mbele wa jengo. Rangi na michoro iliyopakwa kwenye jengo husaidia jengo lifanane na mazingira ya hapo.
Septemba 27, 2018—Jengo la Kusini la Uzalishaji
Baada ya kumwaga sementi, wajenzi hutumia mashine kusawazisha sakafu ili ing’ae na kuwa imara.
Oktoba 4, 2018—Jengo la Ofisi
Picha iliyopigwa kutoka angani upande wa kaskazini-mashariki. Mbele, kikosi cha wajenzi kinasafisha uwanja na kusawaziaha ardhi kupata eneo la kujenga jengo la mapokezi na sehemu ya kuegesha magari. Nguzo kwa ajili ya sehemu ya mapokezi, upande wa kushoto zimekamilika. Majengo ya kaskazini na kusini ya uzalishaji yanaonekana kwa nyuma.
Oktoba 10, 2018—Eneo la Ofisi ya Tawi
Karibu na Jengo la Makazi A, mtaalamu anakagua rekodi za bustani. Kwa kuwa bustani ilisawazishwa mwanzoni, miti na mimea itakuwa imesitawi ujenzi utakapokamilika.
Oktoba 31, 2018—Makazi F
Mafundi wakipaka rangi maalum kwenye sakafu ya kuegesha magari. Mmoja amevaa viatu vya kipekee ambavyo haviachi alama kwenye sakafu. Sakafu iliyopakwa rangi maalum ni ngumu na haiwezi kushika madoa ya mafuta—inafaa kabisa eneo ambalo magari huegeshwa.
Novemba 6, 2018—Jengo la Kusini la Uzalishaji
Mafundi bomba wanapima na kukata minyororo inayotumiwa kuning’niza mivumo ya kuongeza joto katika eneo kubwa la kufanyia kazi.
Novemba 6, 2018—Jengo la Ofisi
Wafanyakazi wakipaka awamu ya kwanza ya rangi ndani ya Jengo la Ofisi. Kifaa kinachoitwa HVAC kilicho na uwezo wa kupasha chumba, kuinginza hewa safi au kupooza chumba kimetokezea kwenye dari ya kila ofisi, na kufunikwa kwa plastiki nyeusi ili kuwa na usalama.
Novemba 8, 2018—Jengo la Ofisi
Wajenzi wanaweka nguzo za chuma juu ya sehemu itakayokuwa mapokezi.
Desemba 7, 2018—Jengo la Ofisi
Wanakandarasi wanatumia mtambo maalum wa kunyanyua vioo nje ya eneo la ukumbi na chumba cha kulia chakula.
Desemba 10, 2018—Jengo la Ofisi
Kikosi cha Habari za Kielektroni kikiweka vifaa vya kuunganisha kwenye ncha za nyaya za kupitisha habari. Nyaya za kupitisha habari zenye urefu wa kilomita 50 zimewekwa chini ya sakafu iliyoinuliwa kwenye kila orofa ya ya Jengo la Ofisi. Sakafu iliyoinuliwa inafanya iwe rahisi kubadili muundo wa ofisi bila kusababisha uharibifu mkubwa.
Desemba 26, 2018—Makazi A
Kikosi cha Kukabiliana na Dharura kikifanya mazoezi ya kumwokoa majeruhi aliyeanguka kutoka kwenye jengo la muda akiwa amefungwa kwa kamba za usalama.
Januari 8, 2019—Jengo la Ofisi
Mshiriki wa Kikosi cha Wafanyakazi akisawazisha kijia kabla ya kuweka vigae. Kandokando ya kijia, trekta linachimba mtaro, na kuandaa sehemu ya kupanda miti ya asili iitwayo hornbeam.
Januari 9, 2019—Jengo la Uzalishaji
Kutokea juu. Mifumo ya kipekee imewekwa juu ya paa la jengo la uzalishaji, na Jengo la Ofisi, ili kubadili mwangaza wa jua kuwa umeme.
Januari 17, 2019—Jengo la Ofisi
Mshiriki wa kikosi cha Kukamilisha anaweka vigae vya sakafu ya chokaa kwenye mwingilio wa orofa ya tatu. Tabaka la rangi ya chungwa linalinda sakafu isipasuke iwapo sehemu iliyo chini itasogea.
Januari 21, 2019—Eneo la kutoa huduma
Wafanyakazi wenye njaa wanachuka chakula cha mchana kwenye chumba cha muda cha kulia chakula. Wafanyakazi katika chumba hiki cha chakula hufanya kazi kwa zamu tatu na kuandaa milo elfu moja hivi kwa siku.
Januari 30, 2019—Jengo la Ofisi
Malori yanaondoa takataka mwishoni mwa eneo la ofisi. Upande wa kulia, mapazia yamewekwa kwenye safu ili kukinga chumba cha chakula kutokana na miale ya jua wakati wa msimu wa baridi kali.
Januari 30, 2019—Jengo la Ofisi
Kikosi cha Kukamilisha kinaweka zulia la vigae, kikisaidiwa na wafanyakazi wa Programu ya Wajitoleaji wa Siku Moja. Kupitia programu hii, makutaniko ya Mashahidi wa Yehova kotekote Uingereza waliombwa kutuma wajitoleaji wanaoweza kusaidia kwa siku moja. Kufikia mwishoni mwa Februari, zaidi ya wajitoleaji 5,500 wanaojitolea kwa siku moja wameshiriki katika mradi huu.
Februari 12, 2019—Jengo la Kusini la Uzalishaji
Wanakandarasi wakijenga ukuta mrefu katikati ya jengo ili kutokeza sehemu mbili. Safu za rangi ya chungwa zilizo sakafuni zinaonyesha sehemu salama ambayo kigari cha kubeba mizigo mizito kinapaswa kupitia.
Februari 20, 2019—Jengo la Ofisi
Wafanyakazi wanadumisha usafi katika eneo huku sakafu iliyoinuliwa ikijengwa kwenye eneo la mapokezi.