WIMBO NA. 94
Kulithamini Neno la Mungu
-
1. Ee, Yehova Baba, twakushukuru,
Kwa kutupa Neno lako la nuru!
Roho iliongoza,
walioandika.
Latupa hekima, twawekwa huru.
-
2. Neno lina nguvu, lapenya moyo.
Linatambua fikira na nia.
Sheria zako njema,
na ni kamilifu.
Zaturekebisha, zatuongoza.
-
3. Nalo Neno lako, latuvutia.
Manabii walilizingatia.
Tujifunzapo Neno,
Tunaimarishwa;
Tunakushukuru, kwa Neno lako!
(Ona pia Zab. 19:9; 119:16, 162; 2 Tim. 3:16; Yak. 5:17; 2 Pet. 1:21.)