WIMBO NA. 12
Mungu Mkuu, Yehova
-
1. Mungu mkuu, unastahili,
Kusifiwa zaidi,
U Mungu mwenye haki.
U Mweza-yote, Mwenye upendo;
U Mungu wa milele.
-
2. Baba twaona, rehema zako.
Tu watu wa mavumbi;
Nawe waturehemu.
Watufadhili, watuongoza,
Daima maishani.
-
3. Mbingu, dunia, zakupa sifa;
Twakusifu kwa nyimbo,
Twakukweza milele.
Mungu mkuu, unastahili.
Pokea sifa zetu.
(Ona pia Kum. 32:4; Met. 16:12; Mt. 6:10; Ufu. 4:11.)