Je, Umejitayarisha kwa Ajili ya Siku Muhimu Zaidi Katika Mwaka?
Je, Umejitayarisha kwa Ajili ya Siku Muhimu Zaidi Katika Mwaka?
SAA chache kabla ya kifo chake, Yesu alianzisha njia ya pekee ya kukumbuka kifo chake. Ukumbusho huo ulikuja kujulikana kama “mlo wa jioni wa Bwana,” au “chakula cha Bwana.” (1 Wakorintho 11:20; Union Version) Akionyesha umuhimu wa tukio hilo, Yesu aliamuru: “Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” (Luka 22:19, Biblia Habari Njema) Je, unatamani kumtii Yesu? Ikiwa ndivyo, basi utauona Ukumbusho wa kifo cha Yesu kuwa siku muhimu zaidi katika mwaka.
Lakini unapaswa kukumbuka tukio hili lini? Na unaweza kuhakikisha jinsi gani kwamba umejitayarisha vizuri kuelewa maana ya tukio hili muhimu? Haya ni maswali ambayo kila Mkristo anapaswa kuyafikiria kwa makini.
Tukio Hili Linapaswa Kukumbukwa Mara Ngapi?
Kwa kawaida sisi hukumbuka matukio muhimu mara moja kwa mwaka. Kwa mfano, ingawa tukio baya la Septemba 11, 2001 (11/9/2001), bado liko katika akili za watu wa Jiji la New York, ambao walipoteza wapendwa wao wakati majengo ya World Trade Center yaliposhambuliwa, tarehe hiyo inapofika kila mwaka, inakuwa na maana ya pekee kwa watu hao.
Vivyo hivyo, katika nyakati za Biblia matukio muhimu yalikumbukwa kila mwaka. (Esta 9:21, 27) Yehova aliwaamuru Waisraeli waadhimishe kila mwaka kukombolewa kwao kimuujiza kutoka utumwani Misri. Biblia inayaita maadhimisho hayo Pasaka, na Waisraeli waliyafanya mara moja kwa mwaka katika siku hususa waliyokombolewa.—Kutoka 12:24-27; 13:10.
Yesu alikuwa amemaliza tu kuadhimisha Pasaka pamoja na mitume wake alipoanzisha mlo wa pekee ambao ungekuwa mfano wa jinsi kifo chake kingepaswa kukumbukwa. (Luka 22:7-20) Pasaka iliadhimishwa kila mwaka. Hivyo, tunaweza kufikia mkataa kwamba tukio hili jipya linaloadhimishwa badala ya Pasaka linapaswa pia kufanywa mara moja kwa mwaka. Lakini tarehe gani?
Tukio Hili Likumbukwe Tarehe Gani?
Ili kujibu swali hilo, tunahitaji kujua mambo mawili. Kwanza, katika nyakati za Biblia siku mpya ilianza jioni, wakati wa kutua kwa jua, na ilimalizika siku iliyofuata wakati wa kutua kwa jua. Kwa hiyo, siku ilianza jioni na kumalizika jioni.—Mambo ya Walawi 23:32.
Pili, Biblia haitumii kalenda tunayotumia leo. Badala ya kutumia miezi yenye majina kama Esta 3:7) Wayahudi walihesabu miezi yao kuanzia mwezi mpya hadi mwezi mpya. Waliadhimisha Pasaka siku ya 14 ya mwezi wa Nisani. (Mambo ya Walawi 23:5; Hesabu 28:16) Siku hiyo, yaani, Nisani 14 inalingana na tarehe ambayo Waroma walimtundika Bwana wetu Yesu Kristo. Alikufa miaka 1,545 baada ya kuadhimishwa kwa Pasaka ya kwanza. Nisani 14 ni tarehe muhimu kama nini!
Machi (Mwezi wa 3) na Aprili, Biblia inaiita miezi hiyo Adari na Nisani. (Lakini ni tarehe gani inayolingana na Nisani 14 katika kalenda yetu ya kisasa? Tunahitaji tu kufanya hesabu rahisi ili kujua tarehe hususa. Nisani 1 huanza mwezi mpya unapotokea na kuonekana Yerusalemu wakati jua linapotua katika siku ambayo urefu wa mchana unakuwa sawa na urefu wa usiku katika majira ya kuchipua kwenye Kizio cha Kaskazini. Ikiwa tutahesabu siku 14 baada ya tukio hilo, tunafika Nisani 14. Kwa kawaida, tarehe hiyo huwa ni siku ya mwezi mpevu. Kwa kutumia njia hiyo ya Biblia ya kuhesabu, Nisani 14 mwaka huu itaanza baada ya jua kutua siku ya Jumapili, Aprili 17, 2011. *
Mwaka huu, Mashahidi wa Yehova wanajiandaa kukutanika pamoja na wale wote ambao wangependa kukumbuka kifo cha Yesu. Wanakualika kwa uchangamfu ushirikiane nao. Tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lenu, ili uweze kujua wakati na mahali ambapo watafanyia mkutano huo. Watakuwa wakiadhimisha tukio hili, si asubuhi wala alasiri, bali jioni baada ya jua kutua. Kwa nini? Kwa sababu kulingana na Biblia, tukio hili linapaswa kuwa “mlo wa jioni.” (1 Wakorintho 11:25) Jioni ya Jumapili, Aprili 17, 2011, ni wakati ambapo tutakumbuka jioni ambayo Yesu alianzisha Ukumbusho huu wa pekee miaka 1,978 iliyopita. Pia, jioni hiyo itakuwa mwanzo wa siku ileile, yaani, Nisani 14, ambayo Yesu alikufa. Hakuna siku nyingine inayofaa kama hiyo ya kukumbuka kifo chake.
Jinsi ya Kujitayarisha
Unaweza kufanya nini sasa ili kujitayarisha kwa ajili ya tukio hili linalofanywa mara moja tu kwa mwaka? Njia moja ni kutafakari kuhusu mambo ambayo Yesu ametufanyia. Kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? * kimewasaidia wengi kuthamini zaidi kifo cha Yesu.—Mathayo 20:28.
Njia nyingine ya kutayarisha mioyo yetu kwa ajili ya tukio hili la pekee ni kusoma kuhusu mambo yaliyotokea kabla na hata siku ya mwisho ya maisha ya Yesu duniani. Katika kurasa zinazofuata utaona chati itakayokusaidia kufanya hivyo. Safu ya kwanza kwenye chati hiyo inaonyesha tarehe za kalenda yetu zinazolingana na tarehe katika kalenda ya nyakati za Biblia. Safu ya pili ina habari fupi kuhusu mambo yaliyotukia katika tarehe hizo, nayo ya tatu inaonyesha mahali ambapo tunaweza kusoma kuhusu matukio hayo katika Vitabu vya Injili na katika kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. *
Tunakutia moyo utenge wakati wa kusoma angalau sehemu fulani za Maandiko yanayoonyesha mambo yaliyotokea katika kila mojawapo ya siku hizo, hadi siku ya Mlo wa Jioni wa Bwana. Jambo hilo litakusaidia kujitayarisha kwa ajili ya siku muhimu zaidi katika mwaka.
[Maelezo ya Chini]
^ fu. 11 Huenda tarehe hii isilingane na ile ya Pasaka inayofuatwa na Wayahudi leo. Kwa nini? Wayahudi wengi leo wanaadhimisha Pasaka katika Nisani 15, wakiamini kwamba amri ile inayopatikana katika Kutoka 12:6 inaelekeza katika tarehe hiyo. (Ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Februari 15, 1990, ukurasa wa 14.) Lakini Yesu aliadhimisha Pasaka katika Nisani 14 kama ilivyoelekezwa katika Sheria ya Musa. Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kufanya hesabu hiyo, ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Kiingereza la Juni 15, 1977 (15/6/1977), ukurasa wa 383-384.
^ fu. 14 Kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova. Ona ukurasa wa 47-56, 206-208. Unaweza kusoma kitabu hiki katika Tovuti ya www.isa4310.com na ya www.watchtower.org.
^ fu. 15 Kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.
[Blabu katika ukurasa wa 22]
Kuadhimisha kifo cha Yesu Jumapili, Aprili 17, 2011
[Chati/Picha katika ukurasa wa 23, 24]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
JUMA LA MWISHO
2011 Jumanne, Aprili 12
▪ Sabato
□ gt 101, fu. 2-4 *
NISANI 9 (yaanza baada ya jua kutua)
Katika nyakati za Biblia siku ilianza jioni, baada ya jua kutua, na ilimalizika siku iliyofuata, baada ya jua kutua
▪ Ashiriki mlo pamoja na Simoni mwenye ukoma
▪ Maria ampaka mafuta ya nardo
▪ Wayahudi wamtembelea Yesu na Lazaro
□ gt 101, fu. 5-9
2011 Alhamisi, Aprili 13
▪ Aingia kwa shangwe ya ushindi jijini Yerusalemu
▪ Afundisha hekaluni
□ gt 102
NISANI 10 (yaanza baada ya jua kutua)
▪ Alala Bethania
2011 Alhamisi, Aprili 14
▪ Afunga safari mapema kwenda Yerusalemu
▪ Asafisha hekalu
▪ Yehova azungumza kutoka mbinguni
□ gt 103, 104
NISANI 11 (yaanza baada ya jua kutua)
2011 Ijumaa, Aprili 15
▪ Afundisha hekaluni, kwa kutumia mifano
▪ Awashutumu Mafarisayo
▪ Amwona mjane akitoa mchango
▪ Atabiri kuanguka kwa Yerusalemu
▪ Atoa ishara ya kuwapo kwake wakati ujao
□ gt 105 hadi 112, fu. 1
NISANI 12 (yaanza baada ya jua kutua)
2011 Jumamosi. Aprili 16
▪ Siku yenye utulivu pamoja na wanafunzi wake huko Bethania
▪ Yuda apanga jinsi ya kumsaliti
□ gt 112, fu. 2-4
NISANI 13 (yaanza baada ya jua kutua)
2011 Jumapili, Aprili 17
▪ Petro na Yohana wafanya matayarisho kwa ajili ya Pasaka
▪ Yesu na mitume wengine kumi wawafuata jioni
□ gt 112, fu. 5 hadi 113, fu. 1
NISANI 14 (yaanza baada ya jua kutua)
▪ Aadhimisha Pasaka
▪ Awaosha mitume mitume wake miguu
▪ Amtaka Yuda aondoke
▪ Aanzisha Ukumbusho wa kifo chake
□ gt 113, fu. 2 hadi mwisho wa sura ya 116
usiku wa manane
2011 Jumatatu, Aprili 18
▪ Asalitiwa na kukamatwa katika bustani Gethsemane
▪ Mitume wakimbia
▪ Ahukumiwa na makuhani wakuu na Sanhedrini
▪ Petro amkana Yesu
□ gt 117 hadi mwisho wa sura ya 120
▪ Asimama mbele ya Sanhedrini tena
▪ Apelekwa kwa Pilato, halafu kwa Herode, kisha arudishwa kwa Pilato
▪ Ahukumiwa kifo na kutundikwa
▪ Afa karibu saa tisa alasiri
▪ Mwili wake waondolewa na kuzikwa
□ gt 121 hadi 127, fu. 7
NISANI 15 (yaanza baada ya jua kutua)
▪ Sabato
2011 Jumanne, Aprili 19
▪ Pilato akubali walinzi wawekwe kwenye kaburi la Yesu
□ gt 127, fu. 8-9
NISANI 16 (yaanza baada ya jua kutua)
2011 Jumatano, Aprili 20
▪ Afufuliwa
▪ Awatokea wanafunzi
□ gt 127, fu. 10 hadi 129, fu. 10
[Maelezo ya Chini]
^ fu. 29 Herufi “gt” zinarejelea kitabu Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Ili kupata chati iliyo na Maandiko mengi zaidi kuhusu siku za mwisho za huduma ya Yesu, ona ukurasa wa 290 wa kitabu “Kila Andiko Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa,” vilivyochapishwa na Mashahidi wa Yehova.