Mazungumzo Ya Familia
Mazungumzo Ya Familia
Ni Nini Kimekosekana Katika Picha Hii?
Soma Yohana 2:13-17. Ni mambo gani manne katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini kisha ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.
1. ․․․․․
2. ․․․․․
3. ․․․․․
4. ․․․․․
ZUNGUMZENI PAMOJA:
Kwa nini Yesu aliwafukuza wanaume hawa kutoka hekaluni?
DOKEZO: Soma Marko 11:17.
Kwa nini lilikuwa kosa kwao kuuza na kununua vitu hekaluni?
DOKEZO: Soma 2 Wakorintho 2:17.
Ili tumpendeze Yehova, tunapaswa kumtumikia tukiwa na nia gani?
DOKEZO: Soma Mathayo 22:36-40; 1 Petro 5:2.
UTENDAJI WA FAMILIA:
Chora au uandike kwenye karatasi jambo fulani unaloweza kufanya linaloonyesha upendo usio na ubinafsi kwa Yehova na watu wengine. Waonyeshe wengine katika familia karatasi yako na mpange jinsi nyote mnavyoweza kushiriki kufanya jambo hilo pamoja.
Kusanya na Ujifunze
Kata, kunja katikati, na uhifadhi
KADI YA BIBLIA 16 TIMOTHEO
MASWALI
A. Jaza mapengo yafuatayo. Mama ya Timotheo, ________, na nyanya yake ________ walimfundisha “maandishi matakatifu” tangu ________.
B. Kijana Timotheo alikubali mwaliko gani wa pekee?
C. Paulo alimwambia hivi Timotheo: “Kama mtoto na baba yake . . .”
[Chati]
4026 K.W.K. Adamu aumbwa
Aliishi katika karne ya kwanza W.K.
1 W.K.
98 W.K. Kitabu cha mwisho cha Biblia kinaandikwa
[Ramani]
Aliishi Listra lakini pia alishuhudiwa vema na akina ndugu katika Ikoniamu
Listra
Ikoniamu
Yerusalemu
TIMOTHEO
MAMBO MACHACHE KUMHUSU
Licha ya kwamba baba yake hakuwa mwamini, alikuja kuwa “kielelezo kwa waaminifu katika kusema, katika mwenendo, katika upendo, katika imani, katika usafi wa kiadili.” (1 Timotheo 4:12) Alifuata shauri hili la Biblia: “Uwe ukijizoeza ujitoaji-kimungu ukiwa ni shabaha yako.” (1 Timotheo 4:7) Timotheo alishirikiana na mtume Paulo kwa angalau miaka 15.
MAJIBU
A. Eunike, Loisi, utoto mchanga.—2 Timotheo 1:5; 3:14, 15.
B. Kusafiri na kutumika pamoja na mtume Paulo.—Matendo 16:1-5.
C. “. . . yeye alitumika pamoja nami katika kuendeleza habari njema.”—Wafilipi 2:22.
Watu na Nchi
5. Majina yetu ni Gabriela na Raul, nina umri wa miaka 6 na Raul ana umri wa miaka 9. Tunaishi Brazili. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Brazili? Ni 467,000, 607,000, au 720,000?
6. Ni alama gani inayoonyesha eneo tunaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, chora alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Brazili.
A
B
C
D
Watoto Watafute Picha
Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.
Ili uchapishe nakala zaidi za “Mazungumzo ya Familia,” nenda kwenye www.isa4310.com/sw
● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 25
MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
1. Yesu alitumia mjeledi, si upanga.
2. Wanaume hao walikuwa wakiuza ng’ombe na kondoo, si nguruwe.
3. Wanaume hao walikuwa wakiuza njiwa, si bundi.
4. Wabadili pesa walikuwa na sarafu, si noti.
5. 720,000.
6. C.