“Ukosefu Mkubwa wa Kuaminiana”
“Ukosefu Mkubwa wa Kuaminiana”
Huko Afrika Magharibi, mvulana mwenye umri wa miaka 12 amelazwa hospitalini kwa sababu ya kupewa dawa bandia ya kutibu malaria ambayo mama yake alinunua kwenye duka la dawa. Daktari mmoja anasema, “Kwa miaka 15 tumekuwa tukipata dawa bandia zikiuzwa.” *
Huko Asia, wazazi wa mvulana mchanga sana wanashtuka kujua kwamba maziwa yaliyoongezwa lishe ambayo walikuwa wakimpa yalikuwa na sumu. Kwa kusikitisha, mvulana huyo anakufa.
Mfanyabiashara mmoja huko Marekani aliyeaminiwa sana amewalaghai wateja wake mabilioni ya dola! Maelfu ya watu wanagundua kwamba malipo yao ya uzeeni yametoweka katika kile ambacho kimetajwa kuwa “upunjaji mbaya zaidi katika karne hii.”
ULIMWENGUNI pote, karibu kila mtu amewahi kusalitiwa na mtu aliyemwamini sana. Hata kuzorota kwa uchumi ulimwenguni kumesababishwa kwa kiasi kikubwa na kile ambacho gazeti la Kifaransa Le Monde lilitaja kuwa “ukosefu mkubwa wa kuaminiana.”
Ni nini kimesababisha ‘ukosefu huo mkubwa wa kuaminiana’? Je, kuna yeyote unayeweza kumwamini?
[Maelezo ya Chini]
^ fu. 2 Ripoti hiyo ilichapishwa katika gazeti Le Figaro, linalochapishiwa Paris, Ufaransa.