Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Maarifa Ni Mengi Lakini Mabadiliko Ni Machache

Maarifa Ni Mengi Lakini Mabadiliko Ni Machache

Maarifa Ni Mengi Lakini Mabadiliko Ni Machache

“Ijapokuwa kumekuwa na maendeleo mengi ya kisayansi, wanadamu hawajafanya mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka elfu mbili iliyopita; kwa hiyo, tungali twahitaji kujitahidi kujifunza kutokana na yaliyopita.” —Kenneth Clark, Civilisation—A Personal View.

BILA shaka, kumekuwa na maendeleo makubwa ya kisayansi katika karne zilizopita. Gazeti la Time linasema kwamba maendeleo hayo “yamewawezesha mamilioni ya watu kuishi maisha ya hali ya juu kuliko katika kipindi kingine chochote.” Maendeleo ya kitiba ni kati ya maendeleo makubwa ambayo yamefanywa. Mwanahistoria Zoé Oldenbourg anasema kwamba katika zama za kati ‘watu walitibiwa bila ustadi na bila huruma. Daktari angeweza kuponya ama kusababisha kifo.’

Nyakati Nyingine Watu Wamekataa Kujifunza

Nyakati nyingine watu wamekataa kujifunza. Kwa mfano, mwishoni mwa miaka ya 1800, madaktari wengi walipuuza uthibitisho wa kutosha kwamba walikuwa wakiwaambukiza wagonjwa wao magonjwa kwa njia fulani. Kwa hiyo waliendelea na mazoea yao hatari na wakakataa kunawa mikono kabla ya kumhudumia mgonjwa mwingine.

Hata hivyo, kulikuwa na maendeleo ya kisayansi na ya kitekinolojia. Basi ni jambo la akili kusema kwamba wanadamu walipaswa kujifunza kutokana na mambo yaliyopita jinsi ambavyo wangeweza kuleta furaha na usalama ulimwenguni. Lakini hawakufanya hivyo.

Hebu fikiria yaliyotukia huko Ulaya katika miaka ya 1600. Kipindi hicho kiliitwa kipindi cha maarifa na akili. Lakini, kama vile Kenneth Clark anavyosema, ‘licha ya maendeleo mengi katika sanaa na sayansi, bado watu waliwanyanyasa wengine bila sababu na watu walipigana kwa ukatili kuliko wakati mwingine wowote.’

Katika nyakati zetu, bado watu hawataki kujifunza kutokana na yaliyopita ili kuepuka kurudia makosa yaleyale yaliyofanywa zamani. Ndiyo sababu inaonekana kwamba uhai wa wanadamu unahatarishwa. Mwandishi Joseph Needham alikata kauli kuwa hali imekuwa hatari sana hivi kwamba ‘twaweza tu kuomba na kutumaini kwamba watu wenye kichaa hawatatumia silaha zinazoweza kuangamiza wanadamu wote na viumbe wote duniani.’

Ni kwa nini kuna jeuri na ukatili mwingi ulimwenguni ijapokuwa wanadamu wana akili nyingi na maarifa mengi? Je, hali hiyo itabadilika? Makala mbili zinazofuata zitazungumzia maswali hayo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

JALADA: Mizinga ya Vita ya Kwanza ya Ulimwengu: U.S. National Archives photo; watu waliouawa katika yale Maangamizi Makubwa ya Vita ya Pili ya Ulimwengu: Robert A. Schmuhl, courtesy of USHMM Photo Archives

Ukurasa wa 2 na wa 3: ndege ya vita ya B-17: USAF photo; mwanamke: Instituto Municipal de Historia, Barcelona; wakimbizi: UN PHOTO 186797/ J. Isaac; mlipuko mkubwa: U.S. Department of Energy photograph