Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Dhahabu” ya Kaskazini

“Dhahabu” ya Kaskazini

“Dhahabu” ya Kaskazini

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI POLAND

TANGU zamani kito aina ya kaharabu kimeitwa dhahabu ya Kaskazini. Kito cha kaharabu kilikuwa bidhaa ya Roma ya kale. Yasemekana kwamba Maliki Nero alimtuma kabaila mmoja anunue kaharabu nchini Poland. Wale waliouza kaharabu, walilipwa nini? Sarafu za dhahabu na za fedha na vilevile bidhaa za kawaida. Yadhaniwa kwamba wale walioeneza Ukristo kufikia Poland katika karne za mapema za Wakati Wetu wa Kawaida, walisafiri kwenye njia ileile ambayo wauzaji wa kaharabu walisafiri.

Baadhi ya watu waliamini kwamba kito cha kaharabu kilikuwa na nguvu za kimzungu. Kwa hiyo, kilitumiwa kutengenezea hirizi za kaharabu ambazo zilidhaniwa kuleta bahati, kumlinda asipatwe na maafa, na kufanikisha uwindaji na vita. Kito cha kaharabu kilitumiwa pia katika kuabudu wafu. Vitu kama visahani vidogo, sanamu ndogo, na vichwa vidogo vya shoka vilitumiwa kuabudu jua, kuabudu wazazi wa kale, na katika ibada ya kuomba mvua na mazao.

Mbali na hayo, kito cha kaharabu kilitumiwa pia kutibu magonjwa mbalimbali. Ilidhaniwa kwamba kuvalia shanga za kaharabu shingoni kungeponya maumivu ya kichwa, shingo na koo, na bangili ya kaharabu ingeponya ugonjwa wa baridi-yabisi. Mafuta mbalimbali ya kuliwaza yenye kaharabu na kileo kilichotiwa kaharabu, vilitumiwa vilevile kutibu wagonjwa. Hata leo wengi huamini kwamba kito cha kaharabu kina uwezo wa kuponya.

Kaharabu humletea Yehova Mungu, aliye Muumba wa vitu vyote, sifa. Mtunga-zaburi alitangaza hivi kwa kufaa: “Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako.”—Zaburi 104:24.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Picha zote: Dziȩki uprzejmości DEJWIS COMPANY; Gdańsk-Polska