Mika 5:1-15
5 “Sasa unajikatakata,Ee binti unayeshambuliwa;Tumezingirwa.+
Wanampiga mwamuzi wa Israeli shavuni kwa fimbo.+
2 Na wewe, Ee Bethlehemu Efratha,+Uliye mdogo sana usiweze kuwa miongoni mwa maelfu ya* Yuda,+Kutoka kwako atatoka kwa ajili yangu yule atakayekuwa mtawala katika Israeli,Ambaye asili yake ni ya tangu nyakati za kale, tangu siku za zamani za kale.
3 Kwa hiyo atawaachaMpaka wakati ambapo mwanamke anayepaswa kuzaa atakapozaa.
Na wale ndugu zake wengine watarudi kwa watu wa Israeli.
4 Atasimama na kuchunga katika nguvu za Yehova,+Katika ukuu wa jina la Yehova Mungu wake.
Nao watakaa kwa usalama,+Kwa maana sasa ukuu wake utafika kwenye miisho ya dunia.+
5 Naye ataleta amani.+
Mwashuru akiivamia nchi yetu na kukanyaga-kanyaga minara yetu yenye ngome,+Tutawainua wachungaji saba dhidi yake, naam, wakuu* wanane wanadamu.
6 Wataichunga nchi ya Ashuru kwa upanga,+Na nchi ya Nimrodi+ kwenye malango yake.
Naye atatuokoa kutoka kwa Mwashuru,+Anapoivamia nchi yetu na kulikanyaga-kanyaga eneo letu.
7 Waliobaki wa Yakobo watakuwa miongoni mwa mataifa mengiKama umande kutoka kwa Yehova,Kama manyunyu ya mvua juu ya mimeaAmbayo hayamtumaini mwanadamuWala kuwangojea wana wa wanadamu.
8 Waliobaki wa Yakobo watakuwa miongoni mwa mataifa,Miongoni mwa mataifa mengi,Kama simba miongoni mwa wanyama wa mwituni,Kama mwanasimba* miongoni mwa makundi ya kondoo,Ambaye hupita na kurukia na kurarua vipandevipande;Wala hakuna yeyote wa kuwaokoa.
9 Mkono wako utainuliwa juu ya maadui wako,Na maadui wako wote wataangamizwa.”
10 “Siku hiyo,” asema Yehova,“Nitawaangamiza kabisa farasi wako na kuharibu magari yako ya vita.
11 Nitaharibu majiji yaliyo katika nchi yakoNa kubomoa ngome zako zote.
12 Nitakomesha ulozi wako,*Na hakuna mchawi yeyote atakayebaki miongoni mwako.+
13 Nitaharibu sanamu zako za kuchongwa na nguzo zako,Nawe hutaiinamia tena kazi ya mikono yako.+
14 Nitang’oa miti yako mitakatifu*+Na kuharibu kabisa majiji yako.
15 Kwa hasira na ghadhabu nitalipiza kisasiDhidi ya mataifa ambayo hayajatii.”
Maelezo ya Chini
^ Au “koo za.”
^ Au “viongozi.”
^ Au “mwanasimba mwenye manyoya marefu shingoni.”
^ Tnn., “kutoka mkononi mwako.”