OKTOBA 2, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kimbunga Boris Chasababisha Mafuriko Makubwa katika Sehemu Mbalimbali za Ulaya ya Kati
Kuanzia Septemba 11, 2024, Kimbunga Boris kilisababisha mvua kubwa na upepo mkali katika sehemu mbalimbali za Ulaya ya Kati. Kimbunga hicho kilipopiga kusini mwa Poland Septemba 12, mvua kubwa ya kipimo cha sentimita 20 hivi ilinyesha ndani ya saa 24 katika baadhi ya maeneo nchini humo, na kusababisha mafuriko katika miji mingi. Mvua hizo kubwa ziliendelea kwa muda mrefu na kuwaacha maelfu ya watu bila umeme. Siku iliyofuata, yaani, Septemba 13, Kimbunga Boris kilisababisha mvua kubwa ya zaidi ya sentimita 50 katika maeneo yaliyo kaskazini mwa Jamhuri ya Cheki na kutokeza uharibifu mkubwa wa nyumba, barabara, na madaraja.
Kisha, Septemba 14, vijiji vingi nchini Romania vilifurika mvua yenye kipimo cha sentimita 25 hivi iliponyesha nchini humo. Mvua hiyo iliharibu nyumba 5,000 hivi na mabwawa mawili katika Jimbo la Galați yakaanza kuvuja. Kimbunga Boris kilifika kaskazini mwa Italia Septemba 18. Katika maeneo mbalimbali, mvua yenye kipimo cha sentimita 30 hivi ilinyesha ndani ya saa 48 na mito ikafurika.
Maelfu ya watu katika nchi hizo nne walilazimika kuhama makazi yao kwa sababu ya kimbunga hicho na wengine 19 hivi walikufa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Jamhuri ya Cheki
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa
Wahubiri 79 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 12 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 2 zilipata uharibifu mdogo
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mdogo
Italia
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa
Wahubiri 63 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 7 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 21 zilipata uharibifu mdogo
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa
Majumba 4 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Poland
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa
Wahubiri 87 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 61 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 85 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 2 ya Ufalme yalipata uharibifu mkubwa
Majumba 8 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Romania
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa
Mhubiri 1 alilazimika kuhama makazi yake
Nyumba 2 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 5 zilipata uharibifu mdogo
Hakuna Majumba ya Ufalme yaliyopata uharibifu wowote
Jitihada za Kutoa Msaada
Halmashauri 6 za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi ili kusimamia kazi ya kutoa msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo wanatoa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa walioathiriwa na mafuriko
Tunapoendelea kusali kwa ajili ya wale walioathiriwa na mafuriko hayo, tuna uhakika kwamba kwa upendo Yehova ataendelea kuwafariji na kuwategemeza.—Isaya 40:11.